CHUO CHA ARDHI TABORA (ARITA)
SERIKALI YA WANACHUO CHUO CHA ARDHI TABORA (ARITASO)
UCHAGUZI WA RAISI WA CHUO CHA ARDHI TABORA (ARITA) 2023/2024
Serikali ya wanachuo chuo cha ardhi Tabora kupitia uongozi wa chuo kutokana na ratiba ya chuo ni wakati wa uchaguzi wa raisi wa chuo cha Ardhi Tabora katika serikali ya wanachuo chuo cha ardhi Tabora (ARITASO): Katika harakati hizo za uchaguzi tume ya uchaguzi serikali ya wanachuo kupitia uongozi wa chuo imesahilisha wagombea watatu kati ya watano wanaowania kiti cha uraisi katika serikali ya wanachuo chuo cha ardhi Tabora.Na wagombea hao ni
1.LUCAS EZEKIEL MURUMBE (Makamu JAMES ATUPELE MPOKI)
2.EDSON JUMBULA MANYAMA(Makamu CATHBET YUDAH LYIMO)
3.DATIUS DEOGRATIUS KIKARUGAA(Mkamu JOSHUA JACKSON NGAYA)
Kwa ufupi wagombea walioorodheshwa hapo juu ndiyo wameshiliwa na Tume ya uchaguzi ya chuo na kutoa tuhusa kwa wagombea kuanza kampeni zao kwa wanchuo wenzao kuanzia tarehe 05/07/2023 saa nane kamili mchana mpaka tarehe 06/07/2023 saa kumi na mbili jioni takribani siku 2 tu. Hivyo na uchaguzi huo utafanyika tarehe 07/07/2023 kuanzia saa 8:00 asbuhi mpaka 6:00 jioni.Mbali na ratiba hiyo ya uchaguzi wagombea wamekuwa na sera zao tofauti tofauti kulingana na matashi ya kila mgombea.
pre by KIF...official
moto sio moto ni balah.................riadha za ushindani wa kampeni za uchaguzi zinazidi kupamba moto chuo cha ardhi Tabora kwa kila mgombea ..kwa kupita kila madarasa ya kozi zote na kunadi sera zao na kuomba kura kwa wanachuo .....yote kwa yote ikiwa kampeni ndogo ambazo zitatamatishwa na kampeni kubwa za ufunguaji na ufungaji wa kampeni..kwa wagombea..kwa ujumla katika ukumbi wa chuo cha Ardhi Tabora.majira ya saa kumi kamili jioni. tarehe 06/07/2023.kampeni zimeisha uchaguzi unaendelea tarehe 07/07/2023 na wanachuo wanajitokeza kwa wingi kupiga kura n'a kusubiri ufungaji wa upigaji kura...mambo ni...moto....kusubiri ..mshindi kutangazwa
Baada ya uchaguzi kutamatika 07/07/2023 na mgombea Mr LUCAS EZEKIELI MURUMBE kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo wa maraisi wa serikali ya wanachuo chuo cha ardhi tabora (ARITASO) kwa idadi ya kura (295) ikiwa idadi ya wapiga kura ni (700) na kura zilizoharibika ni (19)....kwa mwaka 2023/2024 ....taratibu zingine za uteuzi wa baraza la mawaziri zikiwa mbioni kufanyika ili kukamilisha serikali ya wanachuo chuo cha ardhi tabora...."MWANGA WA MAENDELEO ,ELIMU NA MICHEZO" sambamba na "MANENO KIDOGO VITENDO VINGI" ikiwa ni kaulimbiu yake......
N0 |
JINA LA MGOMEA |
IDADI YA KURA ALIZOPATA |
1 |
LUCAS EZEKIEL MURUMBE |
295 |
2 |
EDSON JUMBULA MANYAMA |
195 |
3 |
DATIUS DEOGRATIUS KIKARUGAA |
191 |
|
JUMLA |
681 |
|
IDADI YA WAPIGA KURA NA ZILIZO
HARIBIKA |
700/-19 |